30 Sept 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 29/09/2014

Leo moto wa Injili umewaka katika viwanja vya EAGT Sinai Mwanga - Kigoma, ambapo mpakwa mafuta wa Bwana, mwaimbaji wa kimataifa, mchungaji, mwinjilisti na mpambanaji katika jeshi la Kristo Yesu alikua akimhubiri Kristo hadharani. Katika mkutano huu wa KUNG'OA MAPANDO YASIYOPANDWA NA BWANA NA KUGAWA MAMLAKA uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wana-kigoma walio na kiu ya kusikiliza neno la Bwana. Yesu Kristo ameonekana akitenda kazi na kuangusha ngome za shetani katika mkutano huu.
 Mchungaji mwenyeji, Askofu S. Mloyi  akimpokea Mhubiri Nikodemu Mwahangila katika uanja wa mkutano.

kwaya ya  EAGT Buhoro kutoka Kasulu wakimsifu Bwana

Mchungaji, Mwimbaji na Mhubiri wa mkutano  huu akiimba kabla ya kuanza kuhubiri.

No comments:

Post a Comment