7 Jul 2014

Yaliyojiri mkututano wa CGM jimbo la Kigoma

Leo katika siku ya mwisho ya mkutano mkubwa wa injili hapa Kigoma ulioandaliwa na CGM jimbo la kigoma mambo yalikua moto sana.
Kwaya zilizohudumu ni pamoja na kwaya ya watoto EAGT Sinai, Jeshi kwaya toka FFU, kwaya ya TAG Msufini, Kwaya ya wakinamama Sinai, kwaya ya TAG Buzebazeba, Martha band, na nyingine nyingi.
Mtumishi wa Mungu mchungaji Nicodemus Mwahangila alimalizia kuhubiri katika mkutano huu kwa kufundisha somo la kung'oa mapando ya adui.
Wagonjwa na wenye shida mbalimbali wamefunguliwa kupitia mkutano huu na hakika Yesu Kristo ameonekana akitenda kazi kwa wanakigoma.

Matukio yalivyokua ktika picha.
Askofu Stephen Mloyi akisalimia mkutano

 kwaya ya TAG Msufini wakimsifu Bwana

Martha Band wakihudumu katika mkutano

 Mchungaji Nicodemus Mwahangila (wa kwanza kushoto) muda mfupi kabla ya kusimama madhabahuni
Sehemu ya umati wa wanakigoma waliohudhuria katika  mkutano

Jeshi kwaya kutoka FFU wakimsifu Mungu

 Kwaya ya watoto EAGT Sinai nao walihudumu katika mkutano huu

 watu wakifunguliwa kupitia mkutano huu

mchungaji Mwahangila akihuri katika mkutano huu
  

No comments:

Post a Comment