4 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 3/10/2014

Kwa siku ya tano mfululizo, mchungaji Nikodemu Mwahangila ameendeleza ile 'operation' ya kung'oa kila pando lisilopandwa na Yesu ndani ya mji wa Kigoma.Akiendelea kuhubiri injili ya YESU kristo iletayo uzima tena kwa mifano hai akimuelezea mtumishi wa MUNGU Yohana jinsi bwana YESU alivyokuwa karibu yake wakati akipelekwa katika kisiwa cha patmo akatupwe huko,kwakuwa walikuwa wamechukia baada ya kuonyesha kuwa yupo MUNGU wa kweli na hakuna mwingine zaidi yake.Kwa mfano huo inamaana hata wewe ndugu unayesoma hapa kama kuna watu wanakuchukia yupo MUNGU aishie milele yote anakupenda na anakutabasamulia,wanaopanga mabaya juu yako yeye YESU atashugulika nao.YESU anaendelea kuonekana katika viwanja vya mkutano kwa kuwafungua watu walio fungwa na nguvu za giza na shetani kuendelea kuaibika.Kumbuka na ufahamu ya kuwa hasira na chuki waliyokuwa nayo ndugu zake na Yusufu ndizo zilimpeleka katika kuwa kiongozi tena katika nchi ya ugenini,Hasira na chiki wanazokuwekea watu wasiokupenda ndizo zitakazokupeleka katika hatua nyingine kubwa itakayo wafanya washangae na wajue yupo MUNGU wa kweli apasaye kuabudiwa.
Kwaya ya E.A.G.T-Buhoro kutoka Kasulu wakiimba kumtukuza MUNGU katika mkutano.

 Kwaya ya KYGC wakiimba wambo katika mkutano kumtukuza MUNGU.

Mwimbaji wa nyimbo za injili toka jijini Mbeya BRUNO MWANDELILE akimwimbia MUNGU katika mkutano

Kwaya ya EAGT Sinai - Mwanga Kigoma wakimwimbia MUNGU katika mkutano unaoendelea

Watu wa MUNGU  wakiwa kwenye mkutano kusikiliza MUNGU anasema nini juu ya maisha yao

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Mji kasoro bahari(MOROGORO)Mathias Mwanyamaki(Maarufu kama TRENI MBOVU) akimwimbia MUNGU katika mkutano huu unaoendelea

Mwimbaji wa nyimbo za injili Mathias Mwanyamaki akiimba waimbo wake wa TRENI MBOVU katika mkutano

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mbeya EMMANUEL MGOGO akiimba katika mkutano

Muhuburi wa mkutano wa injili mjini Kigoma Mchungaji NIKODEMU MWHANGILA akiimba katika kutano kabla ya mahubiri

Mchungaji na muhubiri wa mkutano NIKODEMU akihubiri injili ya YESU katika mkutano

Mchungaji na muhubiri wa injili ya YESU ,NIKODEMU MUHANGILA  akiwaongoza watu sala ya toba na kuwaombea kwa MUNGU na wanafunguliwa

Mchungaji na muhuburi wa mkutano akiwaombea watu waliokubali kumpa YESU maisha yao.

No comments:

Post a Comment