5 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 4/10/2014

Mkutano mkubwa wa injili umeendelea tena katika viwanja vya kanisa la EAGT Sinai Mwanga hapa Mjini Kigoma,Mtumishi wa MUNGU Mchungaji na muhubiri wa injili ya YESU Kristo iletayo uzima NIKODEM MWHANGILA anaendelea kumsema YESU na kung'oa mapando yaliyopandwa na shetani kwa watu wa MUNGU, YESU anaonekana akiwafungua watu na kung'oa mapando yoooooooote ambayo shetani kapanda kwa watu.MUNGU ameendelea kuonekana kwa kutumia mtumishi wake,Akihibiri kwa mifano kuntu anasema YESU alipokutana na mtu mwenye pepo kabla hata hajasema neno lolote yakaanza kumuomba msamaha kwa kusema we mtu tuache,au tupe ruhusa tuwaingie wale nguruwe, pepo wakamtoka yule mtu na kuwaingia nguruwe na baada ya wale pepo kuwaingia nguruwe hata wao nguruwe hawakukubali pepo wawaingie waishi kwao zaidi ya nguruwe elfu mbili(2000)wakakimbilia ziwani na kufa wote.Hata sasa YESU Yuleyule bado anatenda mambo makubwa kwa watu wake kwa kuondoa mapepo na majini yooooote ambayo yamepandwa kwa watu na shetani.Injili ya leo ikitoka katika kitabu cha MARKO 4;35-36,Mtumishi na mwandishi wa kitabu hicho akielezea miujiza mikubwa zaidi YESU aliyoitenda wakati huo na ambayo anatenda hata sasa tangu wakati huo.Kama ndugu msomaji kuna mapando yasiyo ya MUNGU kwako Pokeeeeeeeea Uponyaji kwa Jina la YESU.
Waimbaji wa kwaya ya BUHORO wakiimba kumtukuza MUNGU


Kwaya ya EAGT Gungu wakimwimbia MUNGU

Kwaya ya EAGT Sinai Mwanga Kigoma wakimwimbia MUNGU
 

"Wainjilisti wa kesho" kutoka Jeshi kwaya - FFU wakimwinua Yesu

Jeshi kwaya toka FFU wakimsifu Mungu katika mkutano huu

Waimbaji wa nyimbo za Injili Bruno pamoja na Treni mbovu akimsifu BWANA 

Haya sio mashindano ya baiskei bali ni muimbaji Bruno Mwandelile akimsifu Bwana katika mkutano huu


Kwaya ya T.A.G Msufini wakimwainua JEHOVA 

Muimbaji wa nyimbo za Injili Mathias Mwanyamaki a.k.a Treni mbovu akiimba pamoja na watoto katika Mkutano huu. 

'Treni Mbovu' akiwa kati kati ya watoto wakimsifu Bwana.

Emanuel Mgogo akimwinua Bwana.



Mhubiri wa mkutano huu mchungaji Nikodemu Mwahangila akiongoza sala ya toba wale waliokata shauri katika mkutano huu



No comments:

Post a Comment