5 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 4/10/2014

Mkutano mkubwa wa injili umeendelea tena katika viwanja vya kanisa la EAGT Sinai Mwanga hapa Mjini Kigoma,Mtumishi wa MUNGU Mchungaji na muhubiri wa injili ya YESU Kristo iletayo uzima NIKODEM MWHANGILA anaendelea kumsema YESU na kung'oa mapando yaliyopandwa na shetani kwa watu wa MUNGU, YESU anaonekana akiwafungua watu na kung'oa mapando yoooooooote ambayo shetani kapanda kwa watu.MUNGU ameendelea kuonekana kwa kutumia mtumishi wake,Akihibiri kwa mifano kuntu anasema YESU alipokutana na mtu mwenye pepo kabla hata hajasema neno lolote yakaanza kumuomba msamaha kwa kusema we mtu tuache,au tupe ruhusa tuwaingie wale nguruwe, pepo wakamtoka yule mtu na kuwaingia nguruwe na baada ya wale pepo kuwaingia nguruwe hata wao nguruwe hawakukubali pepo wawaingie waishi kwao zaidi ya nguruwe elfu mbili(2000)wakakimbilia ziwani na kufa wote.Hata sasa YESU Yuleyule bado anatenda mambo makubwa kwa watu wake kwa kuondoa mapepo na majini yooooote ambayo yamepandwa kwa watu na shetani.Injili ya leo ikitoka katika kitabu cha MARKO 4;35-36,Mtumishi na mwandishi wa kitabu hicho akielezea miujiza mikubwa zaidi YESU aliyoitenda wakati huo na ambayo anatenda hata sasa tangu wakati huo.Kama ndugu msomaji kuna mapando yasiyo ya MUNGU kwako Pokeeeeeeeea Uponyaji kwa Jina la YESU.
Waimbaji wa kwaya ya BUHORO wakiimba kumtukuza MUNGU


Kwaya ya EAGT Gungu wakimwimbia MUNGU

Kwaya ya EAGT Sinai Mwanga Kigoma wakimwimbia MUNGU
 

"Wainjilisti wa kesho" kutoka Jeshi kwaya - FFU wakimwinua Yesu

Jeshi kwaya toka FFU wakimsifu Mungu katika mkutano huu

Waimbaji wa nyimbo za Injili Bruno pamoja na Treni mbovu akimsifu BWANA 

Haya sio mashindano ya baiskei bali ni muimbaji Bruno Mwandelile akimsifu Bwana katika mkutano huu


Kwaya ya T.A.G Msufini wakimwainua JEHOVA 

Muimbaji wa nyimbo za Injili Mathias Mwanyamaki a.k.a Treni mbovu akiimba pamoja na watoto katika Mkutano huu. 

'Treni Mbovu' akiwa kati kati ya watoto wakimsifu Bwana.

Emanuel Mgogo akimwinua Bwana.



Mhubiri wa mkutano huu mchungaji Nikodemu Mwahangila akiongoza sala ya toba wale waliokata shauri katika mkutano huu



4 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 3/10/2014

Kwa siku ya tano mfululizo, mchungaji Nikodemu Mwahangila ameendeleza ile 'operation' ya kung'oa kila pando lisilopandwa na Yesu ndani ya mji wa Kigoma.Akiendelea kuhubiri injili ya YESU kristo iletayo uzima tena kwa mifano hai akimuelezea mtumishi wa MUNGU Yohana jinsi bwana YESU alivyokuwa karibu yake wakati akipelekwa katika kisiwa cha patmo akatupwe huko,kwakuwa walikuwa wamechukia baada ya kuonyesha kuwa yupo MUNGU wa kweli na hakuna mwingine zaidi yake.Kwa mfano huo inamaana hata wewe ndugu unayesoma hapa kama kuna watu wanakuchukia yupo MUNGU aishie milele yote anakupenda na anakutabasamulia,wanaopanga mabaya juu yako yeye YESU atashugulika nao.YESU anaendelea kuonekana katika viwanja vya mkutano kwa kuwafungua watu walio fungwa na nguvu za giza na shetani kuendelea kuaibika.Kumbuka na ufahamu ya kuwa hasira na chuki waliyokuwa nayo ndugu zake na Yusufu ndizo zilimpeleka katika kuwa kiongozi tena katika nchi ya ugenini,Hasira na chiki wanazokuwekea watu wasiokupenda ndizo zitakazokupeleka katika hatua nyingine kubwa itakayo wafanya washangae na wajue yupo MUNGU wa kweli apasaye kuabudiwa.
Kwaya ya E.A.G.T-Buhoro kutoka Kasulu wakiimba kumtukuza MUNGU katika mkutano.

 Kwaya ya KYGC wakiimba wambo katika mkutano kumtukuza MUNGU.

Mwimbaji wa nyimbo za injili toka jijini Mbeya BRUNO MWANDELILE akimwimbia MUNGU katika mkutano

Kwaya ya EAGT Sinai - Mwanga Kigoma wakimwimbia MUNGU katika mkutano unaoendelea

Watu wa MUNGU  wakiwa kwenye mkutano kusikiliza MUNGU anasema nini juu ya maisha yao

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Mji kasoro bahari(MOROGORO)Mathias Mwanyamaki(Maarufu kama TRENI MBOVU) akimwimbia MUNGU katika mkutano huu unaoendelea

Mwimbaji wa nyimbo za injili Mathias Mwanyamaki akiimba waimbo wake wa TRENI MBOVU katika mkutano

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mbeya EMMANUEL MGOGO akiimba katika mkutano

Muhuburi wa mkutano wa injili mjini Kigoma Mchungaji NIKODEMU MWHANGILA akiimba katika kutano kabla ya mahubiri

Mchungaji na muhubiri wa mkutano NIKODEMU akihubiri injili ya YESU katika mkutano

Mchungaji na muhubiri wa injili ya YESU ,NIKODEMU MUHANGILA  akiwaongoza watu sala ya toba na kuwaombea kwa MUNGU na wanafunguliwa

Mchungaji na muhuburi wa mkutano akiwaombea watu waliokubali kumpa YESU maisha yao.

3 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 2/10/2014

"Operation" ya kungoa kila pando lisilopandwa na BWANA imeendelea tena alhamisi ya leo. Mtumishi wa Mungu, mchungaji Nikodemu Mwahangila aliendelea kumsema Yesu kwa wanakigoma waliohudhuria katika mkutano wa Injili ulioandaliwa na kanisa la E.A.G.T Sinai Mwanga.
Hakika tumemuona Yesu akitenda kazi wazi baada ya mama mmoja anayeishi maeneo ya Mlole kuokotwa alfajiri ya leo(alhamisi) jirani na viwanja vya mkutano. baada ya maombezi na kumpokea Yesu, mama huyo alishuhudia kua alichukuliwa bila kujifahamu toka jana (jumatano) jioni alipokua kwenye biashara zake na fahamu zilimrudia alipokua kanisani akiombewa.
Baadhi ya  kwaya zilizohudumu ni pamoja na  Kwaya kuu ya Sinai, E.A.G.T Buhoro kwaya kutoka Kasulu,
kwaya ya T.A.G Msufini, E.A.G.T Bangwe kwaya, Bruno Mwandelile kutoka Mbeya, Mathias Mwanyamaki (Treni Mbovu), Emanuel Mgogo toka Mbeya na wengine wengi
Jeshi kwaya wakiimba katika mkutano huu

 Kwaya ya E.A.G.T. Sinai wakimtukuza Bwana katika Mkutano.  

T.A.G Msufini nao walikuwepo kumwinua Bwana Yesu

Bruno Mwandelile na Emanuel Mgogo wakimsifu Mungu

Kwaya ya E.A.G.T Bangwe 


Mathias Mwanyamaki (TRENI MBOVU) akimsifu Mungu

Kwaya ya Buhoro wakimwimbia Bwana

Mwimbaji Emanuel Mgogo kutoka Mbeya akiwa jukwaani

Mchungaji Nikodemu Mwahangila akihubiri

Askofu Stephen Mloyi wa E.A.G.T jimbo la Kigoma akizungumza jambo, kulia ni mama aliepotea katika mazingira ya kutatanisha na kuokotwa maeneo ya jirani na viwanja vya mkutano

Baadhi ya watu waliokata shauri katika Mkutano huu

2 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 1/10/2014

Ule moto wa Injili unaoenda sambamba na 'operation' ya kung'oa kila pando lisilopandwa na YAHWE umeendelea jumatano hii tena kwa kasi ya ajabu. Yesu Kristo kupitia mtumishi wake Mchungaji Nikodemu Mwahangila aliendelea kuzivunja ngome za shetani katika mji wa Kigoma na wengi wamemrudia Yesu.
Baadhi ya matukio yaliojiri katika mkutano huu.
Kwaya CGM Sinai wakiimba katika mkutano huu

Kwaya ya E.A.G.T Buhoro kutoka Kasulu wakimwinua Yesu

Kwaya ya E.A.G.T Gungu wakimwimia Yesu katika mkutano huu

Mwimbaji Emanuel Mgogo akiwasili katika viwanja vya mkutano

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bruno Mwandelile akimtukuza Yesu 

Jeshi kwaya kutoka  FFU nao walikuepo kumsifu Mungu

Kwaya ya wenyeji Sinai wakimsifu Mungu kwa njia ya nyimbo

Mwimbaji "TRENI MBOVU" akimwimbia Bwana 

Jukwaa lilikua halitoshi kwa 'TRENI MBOVU' na timu yake

Sehemu ya umati wa wanakigoma waliokusanyika katika mkutano huu

Kwaya ya E.A.G.T Bangwe wakihudumu

Mwimbaji wa kimataifa Emanuel Mgogo akimwimbia Bwana


Mchungaji mwahangila akiimba na wanakigoma kabla ya kuhubiri 



Mathias Mwanyamaki a.k.a Treni mbovu akiimba katika mkutano huu. jukwaa lilikua halitoshii. hebu jionee mwenyewe hapa
Yote haya ni kwa utukufu wa Yesu


Bofya (click) hapo chini kusikiliza sehemu ya mahubiri yaliyohubiriwa leo katika mkutano huu

1 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 30/09/2014

Moto wa Injili mkoani Kigoma umeendelea kuwaka tena katika siku ya pili ya mkutano mkubwa wa injili unaoendelea katika viwanja vya kanisa la E.A.G.T Sinai Mwanga. Mtumishi wa Mungu mchungaji Nikodemu Mwahangila aliendeleza ile oparesheni ya KUNG'OA KILA PANDO LISILOPANDWA NA YAHWE. Tazama kilichojiri katika mkutano huu katika picha
Kwaya ya EAGT Buhoro kutoka kasulu Wakimsifu Bwana

Jeshi kwaya toka E.A.G.T FFU 

Mwaimbaji wa nyimbo za injili Bruno Mwandelile toka Mbeya Akimwimbia Bwana


Kwaya ya E.A.G.T Sinai WAkimwinua Yesu katika mkutano huu 

Mama Askofu Mloyi akisalimia mkutano

Mhubiri wa mkutano huu Mchungaji Nikodemu Mwahangila akihubiri


Mchungaji Nikodemu Mwahangila akiwaongoza sala ya toba watu waliokata shauri katika mkutano huu.


Mathias Mwanyamaki a.k.a Treni Mbovu akimsifu Bwana. Barikiwa na kipande cha video hii

Bofya hapa kusikiliza sehemu ya mahubiri kutoka kwa mchungaji Nikodemu Mwahangila alipokua akihubiri katika mkutano wa leo.