3 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 2/10/2014

"Operation" ya kungoa kila pando lisilopandwa na BWANA imeendelea tena alhamisi ya leo. Mtumishi wa Mungu, mchungaji Nikodemu Mwahangila aliendelea kumsema Yesu kwa wanakigoma waliohudhuria katika mkutano wa Injili ulioandaliwa na kanisa la E.A.G.T Sinai Mwanga.
Hakika tumemuona Yesu akitenda kazi wazi baada ya mama mmoja anayeishi maeneo ya Mlole kuokotwa alfajiri ya leo(alhamisi) jirani na viwanja vya mkutano. baada ya maombezi na kumpokea Yesu, mama huyo alishuhudia kua alichukuliwa bila kujifahamu toka jana (jumatano) jioni alipokua kwenye biashara zake na fahamu zilimrudia alipokua kanisani akiombewa.
Baadhi ya  kwaya zilizohudumu ni pamoja na  Kwaya kuu ya Sinai, E.A.G.T Buhoro kwaya kutoka Kasulu,
kwaya ya T.A.G Msufini, E.A.G.T Bangwe kwaya, Bruno Mwandelile kutoka Mbeya, Mathias Mwanyamaki (Treni Mbovu), Emanuel Mgogo toka Mbeya na wengine wengi
Jeshi kwaya wakiimba katika mkutano huu

 Kwaya ya E.A.G.T. Sinai wakimtukuza Bwana katika Mkutano.  

T.A.G Msufini nao walikuwepo kumwinua Bwana Yesu

Bruno Mwandelile na Emanuel Mgogo wakimsifu Mungu

Kwaya ya E.A.G.T Bangwe 


Mathias Mwanyamaki (TRENI MBOVU) akimsifu Mungu

Kwaya ya Buhoro wakimwimbia Bwana

Mwimbaji Emanuel Mgogo kutoka Mbeya akiwa jukwaani

Mchungaji Nikodemu Mwahangila akihubiri

Askofu Stephen Mloyi wa E.A.G.T jimbo la Kigoma akizungumza jambo, kulia ni mama aliepotea katika mazingira ya kutatanisha na kuokotwa maeneo ya jirani na viwanja vya mkutano

Baadhi ya watu waliokata shauri katika Mkutano huu

No comments:

Post a Comment