1 Dec 2014

YALIYOJILI KATIKA IBADA YA PAMOJA YA MAKANISA YA EAGT MJINI KIGOMA KATIKA PICHA TAREHE 30/11/2014


Ask. Mloyi akiwaombea waumini baraka baada ya ibada

viongozi wa idara wakisikiliza maombi



waumini pia wakisikiliza maombi walipokuwa wakiombewa na Ask. Mloyi
Kwaya ya EAGT gungu ikihudumu

kwaya ya EAGT FFU ikihudumu


Kiongozi wa ibada hiyo na mafundi mitambo nao hawakuwa nyuma

Ask. Mloyi akifafanua jambo kabla ya kuahirisha ibada hiyo kwa maombi

DR. Mgunda akifundisha
Na DR. Mgunda
Alifundisha neno kutoka kitabu cha Yoh. 13:1 – 8
Akizungumzia tendo la Yesu kuwatawaosha miguu wanafunzi wake kwambatendo hili ilikuwa mila iliyokuwepo kwa wayahudi kipindi hicho.Petroalimwambia Yesu huwezi kunitawadha, na Yesu akamjibu kuwa usipotawadhwa nami utakuwa huna shirika nami.
Aliongeza kusema kuwa, watu wengi hawako tayari kuoshwa kwa sababu ya mitazamo na uelewa wao kuwa tofauti. Vumbi la kiroho limo mioyoni mwa watu na ndio maana hata kwenye ibada mbalimbali au makusanyiko ya Kimungu mahudhurio ni madogo sana.inaonyesha ni jinsi gani watu wanavyohitaji kuoshwa vumbi hilo la kiroho ili waweze kuondokana namitazamo iliyowafunga.
Msemaji alisisitiza kuwa Yesu alisema nisipokutawadha/kuosha huna fungu wala sehemu kwangu,kwa hili alisisitiza umuhimu wa kuwa tayari au kumpa Yesu nafasi ya kukuhudumia.
Ubarikiwe na bwana


Waumini wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kikiendelea kwenye ibada hiyo


VIONGOZI WA IDARA MBALIMBALI WAKIFUATILIA KWA MAKINI YALIYOKUWA YAKIENDELEA

Kwaya ya EAGT Sinai ikihudumu katika ibada hiyo
Baadhi ya wachungaji waliohudhuria katika ibada hiyo ya pamoja

Baadhi ya maaskofu wa Jimbo la kigoma Mjini.Kutoka kushoto ni Mch.Douglas Kabogi ambaye ni mwenyeji, katikati ni Ask. Stephen Mloyi na kulia ni Ask mstaafu DR. Mgunda ambaye ndiye alikuwa mnenaji wa neno siku hiyo.

5 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 4/10/2014

Mkutano mkubwa wa injili umeendelea tena katika viwanja vya kanisa la EAGT Sinai Mwanga hapa Mjini Kigoma,Mtumishi wa MUNGU Mchungaji na muhubiri wa injili ya YESU Kristo iletayo uzima NIKODEM MWHANGILA anaendelea kumsema YESU na kung'oa mapando yaliyopandwa na shetani kwa watu wa MUNGU, YESU anaonekana akiwafungua watu na kung'oa mapando yoooooooote ambayo shetani kapanda kwa watu.MUNGU ameendelea kuonekana kwa kutumia mtumishi wake,Akihibiri kwa mifano kuntu anasema YESU alipokutana na mtu mwenye pepo kabla hata hajasema neno lolote yakaanza kumuomba msamaha kwa kusema we mtu tuache,au tupe ruhusa tuwaingie wale nguruwe, pepo wakamtoka yule mtu na kuwaingia nguruwe na baada ya wale pepo kuwaingia nguruwe hata wao nguruwe hawakukubali pepo wawaingie waishi kwao zaidi ya nguruwe elfu mbili(2000)wakakimbilia ziwani na kufa wote.Hata sasa YESU Yuleyule bado anatenda mambo makubwa kwa watu wake kwa kuondoa mapepo na majini yooooote ambayo yamepandwa kwa watu na shetani.Injili ya leo ikitoka katika kitabu cha MARKO 4;35-36,Mtumishi na mwandishi wa kitabu hicho akielezea miujiza mikubwa zaidi YESU aliyoitenda wakati huo na ambayo anatenda hata sasa tangu wakati huo.Kama ndugu msomaji kuna mapando yasiyo ya MUNGU kwako Pokeeeeeeeea Uponyaji kwa Jina la YESU.
Waimbaji wa kwaya ya BUHORO wakiimba kumtukuza MUNGU


Kwaya ya EAGT Gungu wakimwimbia MUNGU

Kwaya ya EAGT Sinai Mwanga Kigoma wakimwimbia MUNGU
 

"Wainjilisti wa kesho" kutoka Jeshi kwaya - FFU wakimwinua Yesu

Jeshi kwaya toka FFU wakimsifu Mungu katika mkutano huu

Waimbaji wa nyimbo za Injili Bruno pamoja na Treni mbovu akimsifu BWANA 

Haya sio mashindano ya baiskei bali ni muimbaji Bruno Mwandelile akimsifu Bwana katika mkutano huu


Kwaya ya T.A.G Msufini wakimwainua JEHOVA 

Muimbaji wa nyimbo za Injili Mathias Mwanyamaki a.k.a Treni mbovu akiimba pamoja na watoto katika Mkutano huu. 

'Treni Mbovu' akiwa kati kati ya watoto wakimsifu Bwana.

Emanuel Mgogo akimwinua Bwana.



Mhubiri wa mkutano huu mchungaji Nikodemu Mwahangila akiongoza sala ya toba wale waliokata shauri katika mkutano huu



4 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 3/10/2014

Kwa siku ya tano mfululizo, mchungaji Nikodemu Mwahangila ameendeleza ile 'operation' ya kung'oa kila pando lisilopandwa na Yesu ndani ya mji wa Kigoma.Akiendelea kuhubiri injili ya YESU kristo iletayo uzima tena kwa mifano hai akimuelezea mtumishi wa MUNGU Yohana jinsi bwana YESU alivyokuwa karibu yake wakati akipelekwa katika kisiwa cha patmo akatupwe huko,kwakuwa walikuwa wamechukia baada ya kuonyesha kuwa yupo MUNGU wa kweli na hakuna mwingine zaidi yake.Kwa mfano huo inamaana hata wewe ndugu unayesoma hapa kama kuna watu wanakuchukia yupo MUNGU aishie milele yote anakupenda na anakutabasamulia,wanaopanga mabaya juu yako yeye YESU atashugulika nao.YESU anaendelea kuonekana katika viwanja vya mkutano kwa kuwafungua watu walio fungwa na nguvu za giza na shetani kuendelea kuaibika.Kumbuka na ufahamu ya kuwa hasira na chuki waliyokuwa nayo ndugu zake na Yusufu ndizo zilimpeleka katika kuwa kiongozi tena katika nchi ya ugenini,Hasira na chiki wanazokuwekea watu wasiokupenda ndizo zitakazokupeleka katika hatua nyingine kubwa itakayo wafanya washangae na wajue yupo MUNGU wa kweli apasaye kuabudiwa.
Kwaya ya E.A.G.T-Buhoro kutoka Kasulu wakiimba kumtukuza MUNGU katika mkutano.

 Kwaya ya KYGC wakiimba wambo katika mkutano kumtukuza MUNGU.

Mwimbaji wa nyimbo za injili toka jijini Mbeya BRUNO MWANDELILE akimwimbia MUNGU katika mkutano

Kwaya ya EAGT Sinai - Mwanga Kigoma wakimwimbia MUNGU katika mkutano unaoendelea

Watu wa MUNGU  wakiwa kwenye mkutano kusikiliza MUNGU anasema nini juu ya maisha yao

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Mji kasoro bahari(MOROGORO)Mathias Mwanyamaki(Maarufu kama TRENI MBOVU) akimwimbia MUNGU katika mkutano huu unaoendelea

Mwimbaji wa nyimbo za injili Mathias Mwanyamaki akiimba waimbo wake wa TRENI MBOVU katika mkutano

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mbeya EMMANUEL MGOGO akiimba katika mkutano

Muhuburi wa mkutano wa injili mjini Kigoma Mchungaji NIKODEMU MWHANGILA akiimba katika kutano kabla ya mahubiri

Mchungaji na muhubiri wa mkutano NIKODEMU akihubiri injili ya YESU katika mkutano

Mchungaji na muhubiri wa injili ya YESU ,NIKODEMU MUHANGILA  akiwaongoza watu sala ya toba na kuwaombea kwa MUNGU na wanafunguliwa

Mchungaji na muhuburi wa mkutano akiwaombea watu waliokubali kumpa YESU maisha yao.

3 Oct 2014

Mkutano wa Injili EAGT Sinai 2/10/2014

"Operation" ya kungoa kila pando lisilopandwa na BWANA imeendelea tena alhamisi ya leo. Mtumishi wa Mungu, mchungaji Nikodemu Mwahangila aliendelea kumsema Yesu kwa wanakigoma waliohudhuria katika mkutano wa Injili ulioandaliwa na kanisa la E.A.G.T Sinai Mwanga.
Hakika tumemuona Yesu akitenda kazi wazi baada ya mama mmoja anayeishi maeneo ya Mlole kuokotwa alfajiri ya leo(alhamisi) jirani na viwanja vya mkutano. baada ya maombezi na kumpokea Yesu, mama huyo alishuhudia kua alichukuliwa bila kujifahamu toka jana (jumatano) jioni alipokua kwenye biashara zake na fahamu zilimrudia alipokua kanisani akiombewa.
Baadhi ya  kwaya zilizohudumu ni pamoja na  Kwaya kuu ya Sinai, E.A.G.T Buhoro kwaya kutoka Kasulu,
kwaya ya T.A.G Msufini, E.A.G.T Bangwe kwaya, Bruno Mwandelile kutoka Mbeya, Mathias Mwanyamaki (Treni Mbovu), Emanuel Mgogo toka Mbeya na wengine wengi
Jeshi kwaya wakiimba katika mkutano huu

 Kwaya ya E.A.G.T. Sinai wakimtukuza Bwana katika Mkutano.  

T.A.G Msufini nao walikuwepo kumwinua Bwana Yesu

Bruno Mwandelile na Emanuel Mgogo wakimsifu Mungu

Kwaya ya E.A.G.T Bangwe 


Mathias Mwanyamaki (TRENI MBOVU) akimsifu Mungu

Kwaya ya Buhoro wakimwimbia Bwana

Mwimbaji Emanuel Mgogo kutoka Mbeya akiwa jukwaani

Mchungaji Nikodemu Mwahangila akihubiri

Askofu Stephen Mloyi wa E.A.G.T jimbo la Kigoma akizungumza jambo, kulia ni mama aliepotea katika mazingira ya kutatanisha na kuokotwa maeneo ya jirani na viwanja vya mkutano

Baadhi ya watu waliokata shauri katika Mkutano huu