5 Jul 2014

Yaliyojiri mkutano wa injili CGM jimbo la Kigoma 04/07/2014

Leo katika mkutano wa injili wa CGM jimbo la Kigoma mambo yalikua Moto! Yesu alihubiriwa wazi wazi bila kificho na wanakigoma wote walishuhudia Yesu Kristo akitenda kazi kupitia mtumishi wake Mchungaji Nicodemus Mwahangila.
Kwaya mbali zilihudumu zikiongozwa na Kwaya ya EAGT Sinai Mwanga pamoja na wageni Ebenezer kwaya kutoka Mito ya Baraka na WWI Temeke zote za Dar es salaam. Kwaya nyingine ni pamoja na kwaya ya EAGT Bangwe, treni mbovu, na nyingine nyingi
WAgonjwa na wenyeshida mbalimbali walikutana na Yesu Mtenda miujiza katika mkutano huu.

Ebenezer kwaya toka Mito ya baraka wakimsifu Mungu 

 Kwaya ya WWI Temeke Wakimwimbia Bwana katika mkutano

 Waimbaji wa Treni mbovu nao walikuepo kumtukuza Bwana 
Kwaya ya EAGT Bangwe wakimwimbia Mungu

Umati wa wanakigoma walio na shauku ya kusikia injili ya Yesu Kristo

Mchungaji Nikodemus Mwahangila akihubiri madhabahuni

BARIKIWA NA YESU!!

No comments:

Post a Comment